Hilda Newton engagement report
@HildaNewton21 - 957K followers on X
Measured over 76 original posts from a 30-day window, last computed on August 27, 2026.
Engagement
A typical post picks up 747 interactions against 957K followers, an engagement rate of 0.078%. Measured over 76 original posts, its engagement rate beats 69% of 3,848 tracked accounts of a similar size, which puts it in the middle of its size range rather than at either end. Posts are seen about 30K times each, and 2.52% of those impressions turn into an interaction. That is about 3.10% of the follower count, which is the gap between an audience on paper and an audience in a timeline. Posting runs at about 4.6 posts a day over the last 30 days, though only 23% of days saw any activity at all. Most posts go out around 10:00 UTC, and Wednesday is the busiest day of the week. Of the 76 posts sampled, 43% carry an image or video. The account's strongest tracked post pulled 1.6K interactions, about 2.2x its own typical post. Recurring topics include #updates_kesi_ya_uhaini, #katibampya, #tanzania.
Measured over 76 original posts from a 30-day window, last computed on August 27, 2026. Recurring tags: #updates_kesi_ya_uhaini, #katibampya, #tanzania.
Compared with accounts its own size
Hilda Newton's engagement rate beats 69% of the tracked X accounts closest to it in follower count (3,848 accounts, accounts of similar size (decile 9 of 10)). A percentile is spread evenly by construction, so 50 really is the middle of that group and 90 really is its top tenth.
On engagement per impression rather than per follower it beats 76% of the same group. When those two numbers disagree, the gap is about how far its posts travel rather than how people react to them.
Where this sits in the catalog
At 0.078%, Hilda Newton sits above the 25th percentile of the 37,320 accounts in this comparison. That places it in the below the median band, which runs 0.012% to 0.081%.
Show the percentile table
| Percentile | Engagement rate |
|---|---|
| 10th percentile | 0.002% |
| 25th percentile | 0.012% |
| 50th percentile | 0.081% |
| 75th percentile | 0.436% |
| 90th percentile | 2.10% |
| 99th percentile | 160.1% |
This ruler is the whole measured catalog, not a size-matched group: it shows where the raw rate falls across every account we can measure, all of which are large. For a like-for-like comparison, read the size-band percentile above instead. See how the bands are built
Posting timing
This account posts most often around 10:00 UTC, and Wednesday is its busiest day of the week. The bars below are the catalog-wide pattern, with this account's own busiest slot marked. They do not show how this account performs at each hour: we keep one aggregate per account, not one per hour, so that measurement does not exist in our data.
Show engagement by hour posted, utc as a table
| Hour (UTC) | Vs author median | Posts |
|---|---|---|
| 00:00 UTC | -1% | 52K |
| 01:00 UTC | -2% | 53K |
| 02:00 UTC | -3% | 51K |
| 03:00 UTC | -4% | 55K |
| 04:00 UTC | -6% | 44K |
| 05:00 UTC | -4% | 43K |
| 06:00 UTC | -4% | 49K |
| 07:00 UTC | -5% | 53K |
| 08:00 UTC | -4% | 62K |
| 09:00 UTC | -3% | 71K |
| 10:00 UTC | -2% | 74K |
| 11:00 UTC | -3% | 80K |
| 12:00 UTC | -2% | 88K |
| 13:00 UTC | -2% | 97K |
| 14:00 UTC | -4% | 100K |
| 15:00 UTC | -2% | 103K |
| 16:00 UTC | -3% | 100K |
| 17:00 UTC | -3% | 93K |
| 18:00 UTC | -2% | 87K |
| 19:00 UTC | -2% | 82K |
| 20:00 UTC | -1% | 76K |
| 21:00 UTC | -1% | 67K |
| 22:00 UTC | -1% | 58K |
| 23:00 UTC | -1% | 52K |
Show engagement by day of week as a table
| Day | Vs author median | Posts |
|---|---|---|
| Sunday | +5% | 235K |
| Monday | 0% | 296K |
| Tuesday | -3% | 292K |
| Wednesday | -1% | 254K |
| Thursday | -2% | 248K |
| Friday | -3% | 256K |
| Saturday | +3% | 230K |
Best tweets
- Aug 24, 20262.2x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 276 Mhe. Lissu anaendelea Anauliza Hayao ya kusema sijui tutaifanyaje Serikali Mmeyatoa wapi? Mlimuuliza nani? Hiyo nia ya mazungumzo yangu yalikuwa ni kuwaelewesha watia nia wetu juu ya matatizo ya mfumo wetu wa Uchaguzi. Mambo ya kuitishia serikali na kwamba tutaifanya nini serikali, kuvuruga Uchaguzi sio kosa na kuzuia uchaguzi na kukinukisha mngeniuliza ningewaambia maana yake ni nini? Nia yetu ilikuwa ni hiyo na tukipeleka kila mahali nia yetu hiyo. Sisi sio Conspirators. Mimi siongozi Chama cha Conspirators, mimi naongoza Chama cha wapigania Demokrasia. Tutakapokutana kesho kutwa nataka niwapitishe kwenye ushahidi ulioletwa kwenu niwapitishe kama unatosha kunyonga mtu. Tuahirishe hadi jumatano. Nawashukuru kwa kunisikiliza. Majaji wakubali ombi la Mhe. Lissu la kuhairisha kesi hadi siku ya Jumatano yani Tarehe 26/08/2026 saa tatu asubuhi Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.1x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Leo Agosti 26, 2026 Last time tuliishia part 276 so leo tunaendelea na -; Part 277 Mwenyekiti ameingia tayari Mahakamani akiwa vibe. Amesema naona wameanza kunyoana wenyewe. Watu ššš Amewaona akina Mzee Lwaitama na Jenerali Ulimwengu anasema nyie Wazee hamjakata moto kama wale wazee wengine. Amemuona Makamu Mwenyekiti Heche anasema Makamu ongeza kupeleka moto. Tunawaona mashahidi watatu wa Mh. Lissu wapo hapa Mahakamani, John Heche, John Mnyika na Amani Golugwa. Majaji wameingia tayari muda huu. Na wakati anaingia watu walikuwa wanaimba mtetezi wa wanyonge kwa sauti na kwa vibe. Nimemuona anaongea na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Wakilli Mahinyila anamuuliza mmeshaandaa mashahidi tayari. Anamjibu kitu anasema haya leo tutamaliza hakuna shida. Inapigwa high court Wanaingia Majaji na kukaa sehemu yao. Anasimama karani Criminal session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Lissu. Anasimama Ajuaye Zengeli wakili wa serikali yupo na Katuga, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa kikundi chote kinaiwakilisha Jamhuri na Lissu yupo anajiwakilisha mwenyewe. Waheshimiwa majaji na mimi niko tayari anajibu Lissu. Na mashahidi wangu wako humu naomba watoke ila wasikae mbali. Majaji wanateta na kucheka kidogo. Makamu Heche, Mnyika, Golugwa na Brenda wanatoka zao nje. Watu wanajiset kwenye viti vyao hapo wanakaaa. Majaji wanateta kidogo kisha wanasema tuendeleee. Mhe. Lissu anasema haitakuwa vibaya mkinikumbusha nilipoishia. Jaji Ndunguru pale ulipomtaja Askofu Pissa. Mhe. Lissu sasa leo nataka nijikite kwenye kesi kama ilivyowasilishwa kwenu na Upande wa Mashitaka. Ushahidi wao walivyouleta, Waheshimiwa Majaji naomba niseme utangulizi ufuatao: 1. Mashahidi walioletwa mbele yenu ni mashahidi wa aina gani na ushahidi wao unapaswa upewe uzito wa aina gani? 2. La pili nitazungumzia ushahidi wenyewe. Ushahidi uliotolewa na mashahidi hawa. Na nitaonesha hakuna kosa la Uhaini na hakuna kosa lolote la jinai kwahiyo hayo ndo mawili ya utangulizi. Sasa nianze na la kwanza kuhusu hao mashahidi. Wakati wa Preliminary hearing upande wa mashitaka ulileta orodha ya mashahidi 30. Ambao walisema hao ndio wataleta ushahidi wa kuthibitisha tuhuma za uhaini dhidi yangu. Upande wa mashitaka haukuleta mashahidi wote hao 30 badala yake walileta mashahidi 17 peke yake. Hao 13 ambao hawakuletwa, hawakuletwa kwasababu muhimu fulani na nitazisema. Hiyo ommission ya hao mashahidi 13 is neither insignificant nore without importance. Sio kwasababu hawana maana na sio kwasababu hawana umuhimu. Nianze na ambao waliletwa. Katika mashahidi 17 walioletwa. Mashahidi 8 ni askari Polisi. Mashahidi 9 waliobaki ni mashahidi wa kificho. Mahakama haiwafahamu majina yao. Haiwafahamu kabisa, haifahamu wanaishi wapi? Haifahamu wanafanya kazi gani na haifahamu chochote zaidi ya majina ya P, P1, P2 P nini huko. Inaweza kuwa tumekuwa nao throughout hapa kesi ikiwa inaendelea kwasababu Mahakama haiwajui na upande wa utetezi hauwajui hata kidogo. Kwahiyo ushahidi wa hao mashahidi 9 ni ushahidi wa watu wasiojulikana na Mahakama wala utetezi, Watu pekeee wanaowajua ni waendesha mashitaka waliowaleta. Part 278 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.1x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 287 Katuga: Turudi kwenye masuala ya wanasheria sasa. Unaijua principle ya constructive possession unaifahamu? Mhe. Lissu: Siifahamu labda niiambie. Katuga: Kwamba mtu anaweza kukutwa na kitu ambacho hana lakini amekihifadhi kwa mtu fulani. Mhe. Lissu: inawezekana ndio Katuga: Unajua case laws unajua kitu kinaitwa constructive publication kwamba una knowledge na control? Mhe. Lissu: Sasa mimi sikuwa na control ya publication hiyo ya Jambo. Watu wanacheka. Huyu KATUGA anapitia wakati mgumu sana. Majibu ya shahidi utadhani yeye ndio Wakili anamuuliza. Watu wanacheka Katuga: Nani alisababisha publication? Mhe. Lissu: Ni PW 17. Hakuna aliyemlazimisha kufanya publication. Angeweza kuamua asipublish. Katuga: PW 17 alisema kwamba tulipaswa sisi kupitia wewe? Mhe. Lissu: Sasa tatizo nyie Serikali mnasema nilipublish mimi wakati shahidi wenu alisema walipublish wao kupitia mimi. Huoni shida hapo wewe? Naomba nikae mvua ya maswali ni kubwa. Watu wanacheka. Anakaa Mh. Lissu. Hajapoteza tabasamu lake lote. Katuga: Ukitoa hotuba kila mtu ana haki ya kuitafsiri anavyoona mwenyewe? Mhe. Lissu: Kweli. Katuga: Maneno kwamba tutazuia uchaguzi, kila mtu ana haki ya kuzuia kwa kadri atakavyoona? Kuvuruga uchaguzi si kila mtu atavuruga anavyoona yeye inafaaa? Mhe. Lissu: Kila mmoja abebe mzigo wake. Sio kazi yangu. Katuga: Unakumbuka P3 alivyosema. Mhe. Lissu: P3 ni nani wewe sema ni PW ngapi huyo P3 wako? Katuga: PW 13 unakumbuka anasema walipanga kurushia watu mawe na kuzuia uchaguzi Mhe. Lissu: Alisema ndio hayo ni yake. Katuga: Uchaguzi upo kisheria? Mhe. Lissu: Ndio lakini uchaguzi sheria zake zinasimamiwa na tume. Katuga: Je kuwarushia mawe na kuwapiga watu ni uvunjifu wa amani? Mhe. Lissu: Sio tu amani ni uvunjifu wa sheria pia. Katuga: Hiyo mihimili mitatu nani ni custodian wa amani? Mhe. Lissu: Ni jeshi la Polisi wako chini ya Serikali. Katuga: Unapotishia kuivunja amani hivyo vitisho huwa vimelengwa kwa nani? Mhe. Lissu: Swali lako ni la hovyo. Katuga: Unapotishia unakuwa umelenga nani? Mhe. Lissu: Nikimlenga huyu Bwana anamuonesha Dr. Nshala kuwa nikimtishia ninakuwa nimelitishia Jeshi la Polisi? Hapana. Katuga: Waheshimiwa wameelewa tuache. Mhe. Lissu: Lazima wawe wameelewa nafikiri sio vilaza. Katuga: Kwenye hayo maneno kwamba mtazuia uchaguzi ulisema itakwua kidemokrasia? Mhe. Lissu: Ungeleta masaa matatu yote ya hotuba ungeona hiyo Demokrasia. Katuga: Upo tayari ikuamini unachokisema hiyo video uko tayari tukuoneshe? Mhe. Lissu: Umeleta takataka mahakama ilikataaa. Mimi siwezi kuwasafishia takataka zenu. Mlileta mambo kienyeji yakakataliwa. Katuga: Kwahiyo uko tayari tuyalete? Mhe. Lissu: Mngeleta wenyewe. Mimi nitaitoa wapi hadi nilete. Katuga: Sasa iambie mahakama demokrasia unayoifahamu wewe kila mtu ana haki ya kufanya anachoona kinamfaaa kwamba siku ya kupiga kura aende anayetaka na asiyetaka asiende. Ni sahihi? Mhe. Lissu: Demokrasia yangu mimi inasema ukiwa hutaki jambo chukua hatua kulizuia kwa njia halali ndio maana maandamano yameruhusiwa kisheria. Katuga: Demokrasia ipi hiyo? Mhe. Lissu: Katiba inasema ukifanya maandamano na kuuzuia uchaguzi ni demokrasia kabisa. Niambie wapi sheria imekataza? Katuga: Haya sawa mjanja wewe. š Katuga: Katiba ndio imekupa mamlaka kufanya kuzuia? Soma ibara ya 30. Kwamba huwezi kutumia haki yako kuzuia haki ya mtu mwingine? Mhe. Lissu: Kwanza nimesema kufanya fujo sio kosa lilipo mahakamani. Na katiba sio ibara 30 pekeee. Ziko ibara nyingi humo. Katuga: haya maswali hayana nia yoyote mbaya si ndio Kaka angu? Mhe. Lissu: Umenishtaki kwa uhaini unasema maswali yako hayana nia yoyote. Wewe vipi wewe? Watu wanacheka. ššš Katuga: Tuendelee au tuishie hapa shahidi? Mhe. Lissu: Unaniomba ushauri? Mnyonga na Mnyongwaji tushauriane nini? Part 288 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.1x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 278 Inawezekana mashahidi hao wa siri ni Mapolisi au mtu yeyote, hao ndio mashahidi wa kesi ya Uhaini. Mashahidi 8 ambao ni Mapolisi hao ni mashahidi wa Jeshi la Polisi linaloongozwa na IGP Camilius Wambura na DCI Ramadhani Kingai ambao nimeonesha kuwa nina ugomvi nao wa zaidi ya miongo miwili. Person vendetta dhidi yangu, Hii vendetta ni neno la kiitaliano lenye maana ya Chuki. Hawa watu wamekuwa na chuki dhidi yangu ndio wameleta hao mashahidi waje kunitolea ushahidi wa uhaini. Waheshimiwa Majaji ushahidi wa Shahidi Na. 1 na Na. 16 PW1 na PW 16, ni ushahidi muhimu sana. Sio kwamba una uzito lakini ni muhimu unaonesha aina ya ushahidi ulioletwa. PW 1 George Bagyemu (ukisikia PW jua ni Prosecution Witness) alisema kwenye ushahidi wake kwamba, Yeye ndie aliyeongoza timu ya wapelelezi wa kesi hii kati ya Tarehe 04 April na Tarehe 08 April, 2025. PW1 kwa maneno mengine alikuwa anaongoza upelelezi siku moja kabla sijakamatwa. PW1 alisema kwenye ushahidi wake in chief na kwenye cross examination kwamba wakati anaongoza timu ya upelelezi kuanzia hiyo Tarehe and 04 alikuwa anawasiliana moja kwa moja na DCI Kingai kwa kupitia Ramadhani Ng'azi Deputy Commissioner of Police. Kwenye Cross Examination nilimuuliza kama aliwahi kuwasiliana hata mara moja na ZCO ambae ni Boss wake akasema hapana. Akasema pia hajawahi kuwasiliana na office ya DPP kwasababu huyu ndie anaratibu upelelezi wa jinai akasema HAPANA. Nilimuuliza kama amewasiliana Regional security officer amewahi kuwasiliana nae? Akasema Hapana. Kwamba mkuu wa usalama wa mkoa alisena hajafanya hivyo. Mtu aliyekubali aliwasiliana nae ni DCI Ramadhani Kingai kupitia kwa DCP Ramadhani Ng'anzi. PW1 alisema aliunda timu tatu za Upelelezi. Ambazo ni 1. Operesheni, 2 inteligentsia na 3. ushauri. Kwenye hizo timu 3 timu ninayotaka kuitolea ushahidi ni timu Oparesheni ambayo alisema ilihusika na ukamataji. Nilimuuliza ni wewe ndio uliyeamuru nikamatwe akasema Hapana yani Kiongozi mkuu wa upelelezi hafahamu nani aliyeamuru nikamatwe. Ilikuwaje nikakamatwa? Akajibu kuwa alipigiwa simu na DCP Ng'anzi kuwa mtuhumiwa amekamatwa Mbinga na analetwa Dar es salaaam. Kumbuka yeye anasema ndie mpelelezi mkuu wakati huo, sasa Waheshimiwa Majaji huyo aliyetoa taarifa kuwa nimekamatwa ni yule ambae alikuwa ni kiunganishi kati yake na DCI Kingai na presumably na IGP Wambura. Sasa ni ushahidi wangu kuwa nilikamatwa kwa amri ya KINGAI DCI na Presumably na IGP Wambura ndio walioamuru nikamatwe na ndio walitengeneza kesi sio hawa hapa anamuonesha Katuga. Na hawa akina Kingai miaka 24 iliyopita wamekuwa kwenye Mkakati wa Kunifunga. Wameshindwa siku zote. Waheshimiwa Majaji hayo aliyoysema PW 1 yalithibitishwa substantially 16 aliyathibitisha ACP Amin Mahamba. Mashahidi wengine ni PW2, PW 3, PW 6, PW 9, PW 12 na PW 15. Ushahidi wao kwa ujumla wao ni ushahidi wa watu wa Ramadhani Kingai na Camilius Wambura. Maafisa wa Polisi ambao wakubwa wao wamekuwa na mkakati wa kunifunga kwa miaka 24. Mtakapofanya majumuisho ya ushahidi huu na wa namna hii hauna thamani yoyote. Ni ushahidi wa mashahidi wenye maslahi unahitaji kuwa corroborated na ushahidi huru. Nataka kusema ndio ushahidi tulionao na nitaileta baadae. Sasa nizungumzie ushahidi wa mashahidi wasiokuwa Polisi. PW4, PW 5, PW7, PW 8, PW 10, PW 11, PW13 na PW 14. Hawa ndio mashahidi ambao hakuna anayewajua isipokuwa prosecutor. Mashahidi wote hawa tuna maelezo yao ya maandishi na maelezo yao ya midomo wakiwa hapa Mahakamani. Isipokuwa PW 1 ndio hatuna ushahidi wake wa maandishi ila wengine wote tunao. Sasa nirudi kwa mashahidi wa kificho ukimwachia PW 4 wengine wote 7 walisema hivi kwa maandishi na wakiwa kizimbani hapa. Part 279 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.0x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 279 Mhe. Lissu anaendelea kutoa utetezi wake. 1. Walipanga njama za kufanya uhalifu wakati wa Uchaguzi mkuu mwaka jana. Wote walisema hivyo kwa maandishi hawa mashahidi wa siri na maelezo hayo yaliandikwa Polisi. (Kupiga watu, kuchoma vitu) ni wao walisema hayo. Na ushahidi huo uko hapo mko nao. 2. Wote hao isipokuwa PW4 walikamatwa na Polisi kwa kufanya njama hizo kwa kufanya fujo na wote walikamatwa kwa hizo siku nne yaani Tarehe 04 na Tarehe 08 April. Polisi waliwajua na kuwakamata wote within four days. 3. Mashahidi wote hao baada ya kukamatwa na Polisi wali confess. Walikiri kuwa tunapanga kufanya vurugu kwenye Uchaguzi, wakiwa kizimbani walisema kwamba walipanga kufanya uhalifu tena walikiri hivyo kwa maandishi 4. Mashahidi ambao walikamatwa kama watuhumiwa wote waliachiwa ili waendeleee kupanga njama yani unamkamata mtu kwa uhalifu na unamuachia. 5. Wote waliitwa na Polisi PW 16 Amin Mahamba na kuwambia kubalini kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu na mkikubali tutawafutia mashitaka. Wahalifu wamekiri mbele ya Polisi, Wakaachiwa na kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu. 6. Wahalifu hao self confessed walitoka Dar es salaam na Dar es salaam Oktoba walikufa watu 182 kwa mujibu wa Jaji Chande. PW 10 and PW 11 Walitoka Arusha na Arusha walikufa watu 53 kwa mujibu wa Jaji Chande. PW13 na PW 14 walitokea Mbeya na huko waliuawa watu 80 kwa mujibu wa Jaji CHANDE. (Polisi walikamata watu waliosema wamepanga kufanya uhalifu Oktoba na wakawaachia na hiyo Oktoba ukatokea huo uhalifu watu hao wakiwa uraiani.) Pw 5 na Pw 7 walitokea Songea na Jaji Chande anasema huko nako walikufa watu ila hawakutaja idadi ya waliokufa Songea. PW 16 Amin Mahamba alisema alikuwa kwenye timu ya wapelelezi walioyachunguza mauaji ya Oktoba 29 na nikamuuliza hao waliosema walipanga kufanya fujo Je mliwachukulia hatua yoyote kwasababu machafuko yalitokea? Akajibu kuwa HAPANA, hakuna hatua walichukua. Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa wahalifu wa aina hii una uzito gani KISHERIA? Huu ndio ushahidi wa Serikali dhidi yangu. Ushahidi wa wahalifu waliokiri tutafanya uhalifu wakaja Mahakamani wakakiri. Wakarudi walikokuwa wanapanga na baadae watu wakauwawa wengi huko mitaani. Ushahidi wa aina hii una uzito gani kwenye kesi ya uhaini? Mashahidi wa aina hii ni totally unreliable. Nitaleta kwa maandishi hoja hizo za kisheria. Waheshimiwa Majaji shitaka linasema nilitengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nikathibitisha nia hiyo kwa kutamka yale maneno maarufu. Anatizama juu Mwenyekiti Lissu na kuonesha hawa watu ni wajinga sana. Ngoja tusikie ataendeleaje hapo.....kuna kaukimya kidogo. š Sasa Waheshimiwa Majaji kuhusiana na shitaka hili na kwa mujibu wa maamuzi ya kisheria tuliyozungumza sana kitu cha muhimu ni uwepo wa nia ya kutenda kosa la uhaini. Ushahidi wa Jamhuri unasemaje kuhusu hiyo nia ya kutenda kosa la uhaini? Mashahidi waliotoa ushahidi kuthibitisha hoja hii ni hawa wafuatao. PW1, PW2, PW16 na PW17 ambae ni P yule mwandishi kwa ridhaa yenu naomba nipatiwe exhibit D1, D15 na D16. Kimya kidogo kinapita. Majaji wanaandika na hizo exhibit zinatafutwa. Ushahidi wa PW 1 George Bagyemu Msaidizi wa Mafwele kuhusiana na nia ya kutenda kosa la uhaini inayodaiwa katika hati ya mashitaka kwenye ushahidi wake alisema kwamba mimi nilitengeneza nia ya kuitishia serikali. Aliona nia ya kutenda kosa la uhaini katika kauli niliyotoa. Nia aliiona kwenye maneno yeye. Waheshimiwa Majaji shahidi mwingine aliyeona nia hiyo ni PW 16 Amin Mahamba. Waheshimiwa Majaji Exhibit D15 maelezo yake Polisi alisema huyu Mahamba akasema hivi "Mimi pamoja na timu nzima ya upelelezi tuliitizama na kuiskiliza video hiyo tukabaini kuna kosa la uhaini na kuchapisha taarifa za uongo." Part 280 itaendelea kwenye post inayofuata Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.0x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 288 Katuga: Pale ambapo kifungu cha Sheria kinatoa adhabu maneno kuwa shall be liable. Ni descretion ya Mahakama? Mhe. Lissu: Hakuna descretion adhabu ni hiyo hiyo. Katuga: Je uko aware na kesi ya Shed Mhagama Mhe. Lissu: Wewe mwenyewe hapo unaangalia kwenye laptop mimi unataka niangalie wapi sasa? Katuga: Omission na Contradiction maana yake nini? Mhe. Lissu: Nipe kamusi nitakupa. Katuga: Unataka Hadi kamusi? Mhe. Lissu: Sasa umesema ni maneno ya kisheria. Sheria huwa inajibiwa kwa nyaraka nipe kamusi nikujibu. Katuga: unaweza kutupa tafsiri ya mkanganyiko na kutokuwepo. Mhe. Lissu: Mkanganyiko na jambo moja lina maelezo tofauti mawili na ommision ni kitu hakikuwepo ila kimeletwa. Katuga: anaenda kupiga soga na wenzake pale. Sasa tusaidie tafsiri ya kifungu cha 163 cha Evidence Act. Je contradicting ipo hapo? Mhe. Lissu: Ipo ndio. Katuga: Umewahi kufungua kesi kwa jina lako? Mhe. Lissu: Nimefungua kupitia chama changu. Katuga: Nimekuuliza wewe Mhe. Lissu: We have done things, we have fought. Zipo vita nyingi tumepambana. Katuga: Mambo ya Jaji Chande umesema mengi Mhe. Lissu: Yapi ya Haki jinai au Oktoba 29? Katuga: ya 29 nilisema. Alisema kuwa matukio ya tar. 29 yalipangwa na kupangwa kulitokana na masuala ya Uchaguzi. Mhe. Lissu: Ndio tume huru na mengine Katuga: Nakuheshimu kuna jambo sitaki kukwambia Mhe. Lissu: Unaniheshimu wapi acha umbea. Unataka kuninyonga unasema unaniheshimu. Msingenishtaki kwa uhaini kama unaniheshimu. Katuga: Taarifa ya Jaji Chande tume ile ilisema machafuko yale yalilenga kuzuia uchaguzi? Mhe. Lissu: Hilo sijui nikumbushe. Katuga: Je unakumbuka sana ulisema watatukamata watanifungulia kesi ya Uhaini. Mhe. Lissu: sikumbuki. Nioneshe Katuga: Ulisema Majaji ni MaCCM Mhe. Lissu: Nakumbuka. Katuga: nitakuwa sahihi hapo ndio nia ilianza kujengwa kwasababu mlisema muandamane ili mchukue dola Mhe. Lissu: Sasa si yangekuwepo kwenye hati ya mashitaka hapo. Mbona hamkuyaweka hayo maneno? Katuga: Waheshimiwa Majaji tunaomba D1 na zingine hadi D16 sasa muda umeisha. Sijui tunafanyaje? Majaji wanaandika. Jaji Ndunguru anasema Tunahairisha kesi hadi kesho saa tatu asubuhi. Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.0x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 285 Katuga: Usiende huko Mhe. Lissu: Naenda kote tu, maandamano najua wewe unataka njia ya Mahakama. Katuga: Sheria ya maandamano umetaja sheria yako? Mhe. Lissu: Ibara ya 20(1) ya Katiba inasema tupinge kwa mikusanyiko na maandamano. Jaji Taratibu jamani tafadhali. Naandika. Mhe. Lissu: Haya mikutano ya hadhara imeruhusiwa kisheria. Katuga: Haya nikupe usome? Mhe. Lissu: Nipatie nisome. Anapatiwa Lissu na anasoma. Inaitwa freedom of association and assembly. Katuga: unamfahamu Francis Dyanabo Mhe. Lissu: Julius Ishengoma Francis Dyanabo namjua alienda Mahakamani kupinga sheria za uchaguzi Katuga: Alishinda? Jaji hebu rudia hapo kwa Dyanabo. Mhe. Lissu: Namfahamu personally Julius Ishengoma Dyanabo personally kwasababu alifungua kesi za kupinga sheria ya uchaguzi kwamba kabla ya kufungua kesi ya uchaguzi unapaswa kuweka kiasi cha pesa. Katuga: Kuhusu Mtikila na mgombea binafsi ilikuwaje? Mhe. Lissu: Sasa usiniingilie nikujibu umekuja vizuri. Mtikila alishinda Mahakama kuu, Mahakama ya rufani ilitengua na baadae akaenda Mahakama ya afrika na wakasema huko kuwa Tanzania iruhusu mgombea binafsi. Hii serikali unayotumikia haijawahi kurekebisha hilo hadi leo. Katuga: Sasa nakuuliza ulisema kifungu cha 39 cha Penal Code umesema mambo ya overt act kinasemaje kuhusu njia ngapi za manifestation. Mhe. Lissu: Ziko mbili. Katuga: Ipi na ipi? Mhe. Lissu: Publication of a writing or printing na overt act or deed. Katuga: inapotumika neno or inamaanisha haya maneno yanatumika in alternative? Mhe. Lissu: yanaweza kufanana na yanaweza yasifanane. In this case yanafanana ni matendo. Katuga: Kwahiyo similarities inamaanisha. Kwamba yako similar. Kwahiyo kati ya neno or au and lipi lilipaswa kutumika. Mhe. Lissu: Kwamba ingesomeka by overt act and overt act. Maana yake nini? Katuga: Haya soma hapo. Mhe. Lissu: Sasa hiki umenipa nini? Chukua haya makaratasi yako. Watu wanacheka. šššš Katuga: Wewe ni Kaka angu umenitangulia kwenye taaluma si ungesoma eneo lenyewe kama nimekufunulia ukurasa tofauti. Mhe. Lissu: Sio kazi yangu mimi ungefungua unapotaka wewe. Katuga: Sasa soma kifungu cha 13 cha Intepretation Act Mhe. Lissu: Anasoma. Katuga: Kwahiyo tuamini nini? Mhe. Lissu: Sheria haitungwi ili iwe absurd Katuga: Ulisema kuna mambo yamekukuta kwenye mapambano yako? Nitakuwa sahihi nikisema kuwa wewe ni mtu mwenye chuki dhidi ya serikali. Mhe. Lissu: Nina chuki na serikali ya nchi hii kwasababu imeonea watu wengi. Katuga: Kwahiyo ulisema yote hayo una chuki na serikali? Mhe. Lissu: Nina chuki dhidi ya uonevu wa serikali. Ninayo chuki dhidi ya serikali sahihi kabisa. Wanaonea sana watu. Katuga: Kama Mwanasiasa nia ya Chama cha siasa ni kushika dola? Mhe. Lissu: Sio nia pekeee ni nia mojawapo. Katuga: Tutakuwa hatumalizi. Mhe. Lissu: Tutamaliza tu. Katuga: mihimili mitatu ya dola ni ipi? Mhe. Lissu: executive, Bunge na Mahakama. Katuga: Kwenye sheria majukumu ya hii mihimili mitatu ni nini? Tuanze na Bunge? Mhe. Lissu: Kutunga Sheria Katuga: sasa mbona ulitaka kusema mengine Mhe. Lissu: Sikutaka uishi kwenye ujinga wa kudhani kazi ya Bunge pekee ni kutunga sheria ziko nyingi sana. Katuga: Kazi ya mahakama je? Mhe. Lissu: Kutafsiri sheria na kutengua sheria. Katuga: Jibu maswali yangu usinielimishe? Mhe. Lissu: Wewe ndio umesema mimi ni kaka yako unataka nikuelimishe hutaki tena muda huu nikuelimishe? Katuga: Kazi ya Serikali ni ipi? Mhe. Lissu: Serikali inaisimamia sheria. Kwahiyo? Katuga: Umenipa jibu? Mhe Lissu: kwahiyo kama nimekupa jibu hivi nyie mnasoma sheria wapi? Katuga: Turudi tena Kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu. Pale kanuni ya adhabu iliposema mtu akitengeneza kitendo kwa nia ya kutishia serikali. Je tafsiri kuna takwa kuwa lazima iwe imetishika? Part 286 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.0x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 281 Mhe. Lissu anaendelea na kutoa utetezi wake. Kwahiyo wenye element ya publication ushahidi ulioletwa na upande wa mashitaka ndo huo. Mashahidi ambao hawakuwepo walisema maneno yalisemwa na ambae alikuwepo hakuna anaposema maneno yalisemwa. Aliyekuwepo anakiri publication alifanya yeye. Usambazaji ni wakwake na sio mtu mwingine. PW 17 aliulizwa wewe ulisikia kauli yoyote ya Kijinai? Akasema HAPANA. Nilimuuliza ulisikia kauli yoyote ya kihaini? jibu lake ni HAPANA. Ushahidi wangu juu ya hiyo publication na intention ni ushahidi wangu mashahidi waliokuja na kusema nimetenda kosa wanajichanganya wanasema mambo tofauti wao wenyewe. Sasa Waheshimiwa Majaji huu Mkanganyiko kati ya maneno yalisemwa au hayakusemwa. Kulikuwa na nia au hakukuwa na nia? Kitu gani kilizungumzwa au hakikuzungumzwa, kungekuwa na video yenyewe tungeweza kutatua huo mgogoro. Wajibu wa kuleta hiyo video ulikuwa ni wajibu wa upande wa mashitaka hawakuleta hiyo video. Mahakama haitakaaa ijue yote yanayosemwa yapo kwenye video ni ya kweli au ni uongo tu. Proof ni video sio maneno na hiyo video haipo. Wao wamechomoa vimaneno viwili vitatu wanataka kusema ni uhaini halafu wameacha maneno yote. Walisema wataleta vielelezo 11, walisema wataleta vingine 9 na visivyokuwa vya maandishi wataleta viwili. Hawajaleta hata kimoja. Sio vya maandishi wale hivyo physical ni maneno matupu, na maneno matupu hayavunji mfupa. Na kwenye uhaini mere words do not constitute overt act. Maneno maneno hayatengenezi uhaini. Khatibu Gandi someni nyie hiyo kesi. Mnafanya nini kwenye ofisi za serikali halafu mnajiita mawakili? Waheshimiwa Majaji kuna vitendo vya ukiukwaji wa taratibu wakati wananikamata na upelelezi wa hili shauri. 1. Ni sheria kwamba National Prosecution Act kwamba Mkurugenzi wa mashitaka wao ndo wanacoordinate criminal investigation. Katuga anasema kwa hatua ya sasa asiingie kwenye sheria huko. Lissu anasema mimi nilikuwa nafanya foundation ya ushahidi wangu tu ninaotaka kutoa. Jaji Ndunguru haya endelea sasa, Tumeelewana nenda direct sasa. Mhe. Lissu Ushahidi Na. 1 na 16 niliwauliza hivi, DPP ndie aliyeratibu huu upelelezi majibu ni hapana. Wakaulizwa tena mwakilishi wa DPP alikuwepo kwenye timu ya upelelezi wakasema hapana lakini PW 16 Akasema alikuwepo mwenye jina la kibantu mmoja. Kwahiyo upelelezi haukumshirikisha DPP. Waheshimiwa Majaji Shahidi Na. 01, 02 na 16 Yaani George, Kaaya na Mahamba waliulizwa kwamba mnatambua kwenye PGO mmeamuliwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kutoa maoni na kufanya mikusanyiko wakaulizwa waoneshe kama walizingatia haki za mtuhumiwa? Niliwaambiwa waoneshe haki zangu kwenye maelezo yao na ushahidi wao hawakuwa na lakusema kuhusu namna walivyolinda haki zangu. NB. ASICHOELEWA KATUGA NA WATU WENGI NAFIKIRI. NI HIVI MHESHIMIWA LISSU SIO TU ANAFANYA KESI YA KUJITETEA. MWENZAO ANAFANYA MKUTANO WA HADHARA KWA HIZI SIKU TATU KUTUONESHA MAMBO YAFUATAYO: 1. Umuhimu wa Katiba Mpya 2. Uchaguzi huru na Haki 3. Uhuru wa Mahakama kiujumla. 4. Uonevu wa Jeshi la Polisi na mabadiliko yanayihitajika kwa jeshi hilo kwani linatumika kubambikia kesi watu. 5. Madaraka makubwa ya Rais 6. Elimu ya Uraia kuhusu wajibu wa raia katika kudai demokrasia. 7. Tume Huru ya Uchaguzi na ubovu wa uchaguzi kihistoria toka uhuru hadi sasa. KWA MANENO MENGINE LISSU ANAWAAMBIA KABLA HAMJANINYONGA NAVIACHIA WOSIA VIZAZI VYANGU JUU YA MAMBO YA KWELI NA AMBAYO YATABAKI KUWA MWIBA MILELE NA MILELE. KWA KIFUPI MH. LISSU YUKO MBELE YA MUDA SANA. ANAWACHEZESHA MCHEZO WASIOJUA. HAYA YATABAKI KWENYE PROCEEDINGS SIKU ZOTE NA VIZAZI VITAYASOMA SIKU ZOTE. Part 282 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.0x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 280 Anasimama Wakili wa Serikali Katuga anasema huu ni utetezi na kielelezo hiyo kilipokelewa kama kielelezo D. Kinapokelewa kuonesha contradiction na kuanza kukirejea kama kielelezo cha kawaida. Kitakuwa na kinyume cha kifungu cha 163 kipo for specific purpose na mkiruhusu tutakitumia dhidi yake. Kitakula pande zote mbili, tunaiomba Mahakama irudi kwenye hiyo purpose ya kukipokea hicho kielelezo. Jaji Ndunguru anaandika Mh. Lissu anacheka ngoja tusubiri majibu ya Lissu hapa. Mhe. Lissu anasema sasa mimi niseme kuwa kwao kama ni furaha mimi kukitumia nataka iwe furaha. Mimi sina shida na wao wayatumie tu, Kielelezo kinahusu kesi hii na Mahakama lazima ikisome ikiangalie. Hamna kielelezo kinachukuliwa kwa ajili ya cross tu peke yake, Waheshimiwa nakitumia kwa sababu kinahusu kesi. Sasa kwa vile wamesema ni furaha yao nashangaa kwanini wanalalamika. Mimi nilikiingiza makusudi ili na wao wakitumie, nashangaa tena hawataki. šššš Watu wanacheka hapa. Kumuelewa Katuga unapaswa kuwa umerogwa au huna akili hata kidogo. Majaji wanateta hapa kama dakika 5 sijui nao wana shida gani huko.š haya ngoja tuone. Jaji Ndunguru ameteta na wenzake kwa muda mrefu sana. Halafu huwa ana tabia sana ya kuzungumza na huyu Jaji Karyemaha kwa muda mrefu sana. Sijui huwa anaongea nae nini? Huyu Jaji Kiwonde ambae yuko kushoto kwa Ndunguru yeye ni kama huwa hana habari kabisa. Jaji Ndunguru anasema kwa vile kielelezo kimeingia hatuwezi kusema tunazuia matumizi ya hicho kilelezo. Kwahiyo wewe endelea tu, kelelezo tayari kipo Mahakamani we kitumie. Mhe. Lissu anasema sawa naendelea. Amin Mahamba amesema kuwa mimi pamoja na timu tulitazama video na kuona makosa ya uhaini na kusambaza taarifa za uongo. Kwahiyo PW 16 aliona nia ya kutenda kosa akiwa na PW 1 hawa waliona nia. PW2 na PW 17 Je waliona nia? Waheshimiwa Majaji kwa mujibu wa kielelezo D1 John Kaaya anasema katika picha mjongeo niliona Tundu Lissu akitamka matamshi yenye viashiria vya jinai. Hakuna mahali kokote alipozungumzia uhaini, kosa la uhaini na nia ya uhaini. Aliona viashiria vya jinai. PW 17 anasema kwenye maelezo yake anasema hivi. Katika mkutano huo masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni masuala kuhusu Uchaguzi Mkuu na agenda yao ya No reforms, No election na matatizo yao wanayokumbana nayo kwenye Uchaguzi. Huyu yeye hakuna uhaini aliouona hata mmoja. Anasema alituona tunazungumzia No Reforms No Election na Matatizo tunayokumbana nayo, hakuna uhaini aliousema kabisa. PW 17 ndie shahidi pekee aliyekuwepo kwenye mkutano na hakuona kosa lolote wala uhaini. Hoja ya pili inayogombaniwa kwenye kesi hii ni manifestation ya hiyo nia. Maneno ni haya wanasema kitu kimoja hapa, msimamo huu unaashiria uasi ........ anayasoma yote. Yanayodaiwa kusemwa ndio maneno hayo. Sasa ushahidi unasemaje kuhusu haya maneno? Kuhusiana na hayo maneno, ushahidi wa PW1, PW2 na PW 16 unafanana na mashahidi wote hao wanasema kuwa waliona hiyo video yenye maneno hayo. Na ushahidi wao wamesema mimi ndie niliyechapisha na kuyapeleka Jambo TV. Ushahidi wa PW 17 the eye witness unasemaje? Shahidi Na. 17 wa upande wa mashitaka kwenye maelezo yake D16 anasema hivi katika mkutano huo masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni kuhusu uchaguzi mkuu na mambo ya No Reforms No Election. Hakuna kokote kwenye D15, hakuyaona hayo maneno hakuyasikia, hajayaandika wala hajayasema hapa. Aliyekuwepo hajayaona, hajayasikia kwasababu hajayaandika na hajayasema. Angeyasikia angesema, angeyaona angeyaandika. PW17 alisema hapa Mahakamani na iko kwenye D16 kwamba yeye ndio alipiga picha na kurusha akiwa na wenzake wanne wakitumia camera za SON. Wote ni wafanyakazi wa JAMBO TV. Walirusha mkutano huo ukiwa Live. PW17 alisema kwa maandishi na hapa Mahakamani pia kuwa yeye ndie aliyehifadhi hizo video kwenye mtandao wa Jambo kule Youtube, X na instagram. Alisema yeye sio mimi. Part 281 itaendelea kwenye post inayofuata Naomba Repost yako.
- Aug 26, 20262.0x their median
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 283 Wote wameongeza mambo kwa mdomo ambayo kwenye maandishi hayapo kabisa. Wameongeza yasiyokuwemo kwenye maelezo yao. Ni ushahidi wangu kwamba ushahidi wa maneno unaotofautiana na ushahidi wa maandishi kwenye jambo hilo hilo ni ushahidi usioaminika. Ndio kusema ushahidi wote wa mashahidi wote wa upande wa mashitaka hauaminiki. PW1,2,3,6,9,12 and 16 hawa wote ni mapolisi na waliandika maelezo polisi wenyewe na wakajikanya wenyewe na kujishuhudia wenyewe. Niliwauliza ni sheria gani iliwaruhusu wafanye hivi wakadai ndivyo huwa wanafanya mapolisi. Sasa ni ushahidi wangu kuwa Mapolisi wanafanya mambo kienyeji na vielelezo D1,2,5,8,12 wote walijaindika ni polisi mmoja tu ndio aliandikwa na polisi mwenzake kwa mashahidi wote walioletwa na Jamhuri. Waheshimiwa Majaji wale Mapolisi wa Ruvuma waliandikwa na mapolisi wengine lakini hawakuletwa. Wangewaleta njngewathibitishia kuwa maelezo yao yaliandikwa kwa usahihi. Kwahiyo ushahidi wangu ni huo. Nimemaliza ingawa nimevuta vuta kidogo. Majaji wanaandika. Jaji Ndunguru: Sasa hawa ambao hawajaletwa mahakamani unasemaje sasa? Mhe. Lissu : Wangeletwa tungethibitisha taratibu za kuandika maelezo huwa ukoje. Kwahiyo ni ushahidi unreliable huu unatakiwa kwa kesi kubwa kama hii. Ajuaye Wakili wa Serikali anasema tunaomba health break kabla ya kuanza cross exanination. Naomba repost yako.
Ranked by total interactions across everything we have tracked for this account, which is a longer history than the 30-day window the rates above use. The multiple compares each post to this account's own median.
Recurring topics
The most frequent hashtags in the sampled posts. They describe what this account writes about; they are not a performance signal, and the catalog-wide breakdown on the hub shows how little hashtag count moves.
Buy or sell X accounts - escrow-protected
PlayerSells is an escrow marketplace for X accounts. Every deal is protected, with no middleman risk.
Reading these numbers
A typical post picks up 747 interactions against 957K followers, an engagement rate of 0.078%. Measured over 76 original posts, its engagement rate beats 69% of 3,848 tracked accounts of a similar size, which puts it in the middle of its size range rather than at either end. Posts are seen about 30K times each, and 2.52% of those impressions turn into an interaction. That is about 3.10% of the follower count, which is the gap between an audience on paper and an audience in a timeline. Posting runs at about 4.6 posts a day over the last 30 days, though only 23% of days saw any activity at all. Most posts go out around 10:00 UTC, and Wednesday is the busiest day of the week. Of the 76 posts sampled, 43% carry an image or video. The account's strongest tracked post pulled 1.6K interactions, about 2.2x its own typical post. Recurring topics include #updates_kesi_ya_uhaini, #katibampya, #tanzania.
- What is Hilda Newton's engagement rate on X?
- Hilda Newton (@HildaNewton21) has an engagement rate of 0.078%, based on the median interactions across 76 original posts from the last 30 days against 957,406 followers. Replies, reposts and quote-posts of other people are excluded from that sample.
- Is that a good engagement rate?
- At 0.078%, Hilda Newton sits above the 25th percentile of the 37,320 accounts in this comparison. Those comparison accounts are all large ones, because our scanning cadence is weighted towards big accounts, so this is a ranking among peers of similar scale rather than a ranking across X.
- Does @HildaNewton21 have real engagement?
- Its engagement rate beats 69% of the tracked X accounts closest to it in follower count (3,848 accounts), which puts it in the middle of its size range group. Ranking inside a size band matters because engagement rate falls as accounts grow, so a raw rate would mostly re-measure the follower count. It is a starting point for a look at follower quality, not a verdict on it.
- When does @HildaNewton21 post?
- Most posts go out around 10:00 UTC, and Wednesday is its busiest day, at roughly 4.6 posts per day across the measured window.